Sio kitu cha ajabu kusikia wasanii wakiwarusha wanamichezo kwenye ngoma
zao. Hiki kitu kimeanza muda mrefu sana ndani ya Africa hadi nje ya
Africa. Mmoja kati ya wanamichezao waliohi kutajwa sana
kwenye nyimbo za
HipHop huko marekani ni Michael Jordan au M.J kama wanavyomuita.
Tumeongea na Diamond Platinumz ambapo yeye na wasanii wake wa WCB
wamekua wakitaja majina ya wana michezo mara kadhaa kwenye ngoma zao
hasa Ronaldo na Mbwana Samatta.
Diamond tulipomuuliza kuna faida gani kwake na kipi kinamvutia kutaja
majina ya wachezaji hao kwenye ngoma zake. Jibu lilikua hili “Hata kama
mtu anafanya kazi kiasi gani kama jamii haijamkubali basi bado ana kazi
ya ziada ya kufanya hadi akubalike.”
Aliendelea “Sasa mimi nawataja watu ambao wamefanikiwa kukubalika na
jamii, ukiangalia watu kama Ronaldo na Samatta inaongeza chachu ya
nyimbo na kupendwa zaidi. Hata wao pia wanafarijika kuona kwamba sisi
kwa sisi pia tunakubaliana kwa kila kitu tunachofanya.
Jumatano, 4 Januari 2017
New
HILI ni jibu la Diamond kuhusu kwanini anataja majina ya wacheza soka kwenye ngoma zake
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
TUAMBIE