Waziri wa ulinzi wa Ufaransa,
amesema mitandao ya idara za ulinzi za nchi zilishambuliwa mara 24,000
mwaka jana peke yake lakini udukuzi huo ulizimwa.
Jean Yves-Le Drian, alisema udukuzi kama huo unaongezeka mara dufu kila mwaka.
Alionya kuwa miundo mbinu ya taifa iko kwenye hatari, na kwamba kunaweza kufanywa jaribio la kuchafua uchaguzi wa mwaka huu.
Bwana Le Drian amekuwa akisimamia mabadiliko makubwa katika mifumo ya
mitandao ya Ufaransa, ambapo mkuu wa jeshi ataongoza operesheni mpya za
komputa, Cybercom.
Waziri huyo wa ulinzi alisema hayo
alipozungumza na gazeti moja la Ufaransa, Le Journal du Dimanche, baada
ya idara za usalama za Marekani, kusema kuwa Urusi ilijaribu kuingilia
kati uchaguzi wa rais wa Marekani jambo ambalo Urusi inakanusha.
Raia wa Los Angeles ambao ndio
majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood' waliamka mwaka
mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu umebadilishwa
na kuwa 'Hollyweed'.
Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti
kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na kwamba
wanaendelea na uchunguzi.
Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45.
Wapiga
kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika
kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8
Novemba.
Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo.
Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.
Kampuni moja ya Israel imesema ndege
isiyokuwa na rubani, ambayo ilikamilisha safari yake ya kwanza kabisa
ikipaa juu ya maeneo tambarare mwezi Novemba, huenda ikaanza kutumika
rasmi kufikia 2020.
Ndege hiyo imeundwa na kufanyiwa kazi kwa
kipindi cha miaka 15, lengo likiwa kutumika katika juhudi za uokoaji au
shughuli za kijeshi.
Ndege hiyo ambayo inafahamika kwa sasa kama
Sio kitu cha ajabu kusikia wasanii wakiwarusha wanamichezo kwenye ngoma
zao. Hiki kitu kimeanza muda mrefu sana ndani ya Africa hadi nje ya
Africa. Mmoja kati ya wanamichezao waliohi kutajwa sana
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani
la Guantanamo Bay, Cuba.
Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni "watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena".
Rais Barack Obama alikuwa ameapa kuwa angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo.
Kwa
sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema
baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao kabla ya tarehe
20 Januari.