Jumatatu, 6 Machi 2017

Usimshauri mtoto wako kufanya siasa, huu mchezo unahitaji… – Mrisho Mpoto

by on 17:24
Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amewataadharisha wazazi kuacha kuwashauri watoto wao kuingia kwenye siasa.
Mtunzi huyo mahiri ya mashairi ya Kiswahili ambaye aliwahi kutajwa na vyombo vya habari kutaka kugombea ubunge katika uchaguzi iliopita wa mwaka 2015, amekuwa akichambua baadhi ya matukio yanatokea nchini.
Jumatatu hii ameibuka na kuwashauri wazazi kuacha kuwashauri watoto wao kuingia kwenye siasa kwa madai siasa siyo ishu ya lelemama.
“Hizi ni salaam zangu kwa kina mama wote wenye watoto tumboni, na wale waliokua leba. Pls pls wakijifungua naomba wasiwashauri watoto wao kufanya siasa huu mchezo unahitaji uwe na roho ngumu kama za wale #shilawadu,” aliandika msanii huyo Instagram.
Mwanamashairi huko mbioni kuachia project yake mpya.

Jumanne, 10 Januari 2017

Jumatatu, 9 Januari 2017

Jumapili, 8 Januari 2017

idara za ulinzi za Ufaransa zilishambuliwa mara 24,000 2....2016

by on 21:28
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, amesema mitandao ya idara za ulinzi za nchi zilishambuliwa mara 24,000 mwaka jana peke yake lakini udukuzi huo ulizimwa.
Jean Yves-Le Drian, alisema udukuzi kama huo unaongezeka mara dufu kila mwaka.
Alionya kuwa miundo mbinu ya taifa iko kwenye hatari, na kwamba kunaweza kufanywa jaribio la kuchafua uchaguzi wa mwaka huu.
Bwana Le Drian amekuwa akisimamia mabadiliko makubwa katika mifumo ya mitandao ya Ufaransa, ambapo mkuu wa jeshi ataongoza operesheni mpya za komputa, Cybercom.
Waziri huyo wa ulinzi alisema hayo alipozungumza na gazeti moja la Ufaransa, Le Journal du Dimanche, baada ya idara za usalama za Marekani, kusema kuwa Urusi ilijaribu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa Marekani jambo ambalo Urusi inakanusha.

Ijumaa, 6 Januari 2017

Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed'

by on 15:44

Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed'

Raia wa Los Angeles ambao ndio majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood' waliamka mwaka mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'.
Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45.
Wapiga kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8 Novemba.
Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo.
Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.

Ndege zisizo na marubani kubeba abiria 'kufikia 2020'

by on 12:04
Kampuni moja ya Israel imesema ndege isiyokuwa na rubani, ambayo ilikamilisha safari yake ya kwanza kabisa ikipaa juu ya maeneo tambarare mwezi Novemba, huenda ikaanza kutumika rasmi kufikia 2020.
Ndege hiyo imeundwa na kufanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka 15, lengo likiwa kutumika katika juhudi za uokoaji au shughuli za kijeshi.
Ndege hiyo ambayo inafahamika kwa sasa kama

Jumatano, 4 Januari 2017

Donald Trump asema wafungwa hawafai kuachiliwa Guantanamo Bay

by on 16:51


Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani la Guantanamo Bay, Cuba.
Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni "watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena".
Rais Barack Obama alikuwa ameapa kuwa angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo.
Kwa sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao kabla ya tarehe 20 Januari.

Jumanne, 3 Januari 2017

Theme Support