Jumatatu, 31 Machi 2014

by on 15:32

USAFIRI WA KUSINI UTATUMALIZA

Mwendo kasi wa magari barabara ya kwenda kusini wasababisha ajali mbaya Kibiti wilaya ya Rufiji mkoani Pwani na kusababisha vifo vya watu 22,ajali hii imeusisha magari yapatayao tano moja ikiwa gari ndogo ya abiria (haice )

Jumatatu, 24 Machi 2014

Jumapili, 23 Machi 2014

ONGEZA NGUVU ZA KIUME

by on 21:06

 VYAKULA VINAVYOONGEZA UWEZO KATIKA TENDO LA NDOA

URAFIKI,MAHUSIANO,UCHUMBA NA NDO

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuonge
za majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa

Alhamisi, 6 Machi 2014

UTABIRI WA MVUA KUBWA UKANDA WA PWANI

by on 12:12
BY MWANANCHI MEDIA

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri kuwa mvua kubwa zitanyesha hasa maeneo ya ukanda wa pwani huku ikitahadharisha uwezekano mkubwa kusababisha maafa.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema jana kuwa utabiri huo unaonyesha kuwa maeneo mengi zaidi ya nchi yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani... “Hata shughuli za kilimo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo.”
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari TMA pia imewahadharisha watumiaji wa bahari juu ya mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kusababisha bahari kuchafuka.
Taarifa hiyo imesema kunatarajiwa kuwapo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50, kati ya jana na kesho ambazo zitanyesha mfululizo na kwamba huenda zikasababisha madhara katika ukanda wote wa pwani.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa mvua hizo zinasababishwa na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa Mashariki mwa Bahari ya Hindi, sanjari na kusogea haraka kwa mvua za masika hivyo kuongeza kiwango cha unyevunyevu kuelekea ukanda wa pwani.
Mikoa iliyopo katika ukanda huo ambayo inaweza kuathiriwa na mabadiliko hayo ya hali ya hewa ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na Zanzibar.
“TMA inazitaka mamlaka zinazohusiana na majanga kuchukua hadhari zinazostahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo,” ilisema taarifa hiyo.
Katika taarifa ya tathmini ya mvua za msimu kuanzia Machi hadi Mei, mwaka huu iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita, Mamlaka hiyo ilizitaka menejimenti za maafa na wadau wa sekta ya afya, kuchukua hatua za hadhari kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kutokea kwa kuwa baadhi ya maeneo yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.

Israel yaikamata meli ya Iran iliyobeba silaha nzito

by on 02:20

Israel yaikamata meli ya Iran iliyobeba silaha.

Israel imesema jeshi lake la baharini limeikamata meli ya Iran katika bahari ya Sham, ambayo ilikuwa ikisafirisha maroketi ya kisasa kwa kundi kipalestina la Hamas linaloudhibiti Ukanda wa Gaza. Msemaji wa jeshi la Israel amesema maroketi hayo ni aina ya M-302 yaliyotengenezwa nchini Syria, ambayo yanaweza kupiga shabaha iliyo umbali wa km 160.
Msemaji huyo amesema maroketi hayo yangeiimarisha Hamas kwa kuipa uwezo wa kupiga maeneo karibu yote ndani ya Israel. Meli hiyo ilikuwa ikipeperusha bendera ya Panama, kituo chake cha mwisho kikiwa Port Said nchini Sudan.
Meli za kivita za Israel zinaisindikiza meli hiyo yenye silaha ambayo imebadilishiwa njia na kuelekezwa kwenye bandari ya Eilat nchini Israel. Taarifa za jeshi la Israel zinaeleza kuwa mashirika ya kijasusi ya nchi hiyo yamekuwa yakiifuatilia meli hiyo kwa miezi kadhaa.

Theme Support