
Staa
wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul’Diamond Platinumz’amewachana wasanii
wenzake wanaotafuta bifu na yeye na kusema kuwa amesikitishwa na baadhi
ya wasanii wanaolazimisha kutengezeza ugomvi kilazima bila sababu za
msingi.

Kupitia
account yake ya Instagram Diamond aliandika kuwa…kiukweli, nasikitishwa
sana jinsi baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea
ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu…
Aidha aliongeza kuwa kuna wasanii wengine wamekuwa wakisema kuwa amewatusi kwenye Media, Mara amepost kuwakashifu..
Alimalizia kwa kusema kuwa yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa
Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu
kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui
"sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina
tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu...
Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na
kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu
wanataka kazi!Alimalizia kuandika kwenye Instagram
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
TUAMBIE